ACCRA: Rais wa Ujerumani Horst Köhler atoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubadilisha mtazamo dhidi ya Afrika. | Habari za Ulimwengu | DW | 14.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ACCRA: Rais wa Ujerumani Horst Köhler atoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubadilisha mtazamo dhidi ya Afrika.

Rais wa Ujerumani, Horst Köhler aliye ziarani nchini Ghana, ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kubadilisha mtazamo wake dhidi ya Afrika.

Rais Horst Köhler, ambaye alikuwa akizungumza katika kikao cha siku mbili kuhusu ushirikiano kati ya Ujerumani na Afrika, ameshutumu baadhi ya kampuni za Ujerumani zinazoshiriki ufisadi barani humo.

Rais Köhler alitoa wito kwa Ulaya kuendelea kununua bidhaa kutoka Afrika huku akizingatia zaidi athari mbaya ya sera za uvuvi barani Ulaya.

Kikao hicho kimeandaliwa kwa niaba ya mkakati wa ushirikiano na Afrika ulioanzishwa na Rais Horst Köhler.

Kikao cha kwanza kama hicho kiliandaliwa nchini Ujerumani mwezi Novemba mwaka elfu mbili na tano karibu na Bonn.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com