1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA: Rais Köhler aendelea na ziara yake nchini Ghana

12 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbP

Ziara ya rais wa Ujerumani Hörst Kohler nchini Ghana imeingia siku yake ya pili hii leo. Kufuatia mkutano na rais wa Ghana John Kufuor, rais Köhler ametaka kuwepo ushirikiano wa karibu baina ya mataifa ya Ulaya na Afrika.

Rais John Kufuor wa Ghana amesema, ´Ujumbe anaotaka kuutoa kupitia ushirikiano anaoupigia debe hasa na vijana ni kumfanya kila mtu ahisi sote tuko pamoja na sawa kama binadamu. Tukilielewa hilo kutakuwa na hisia miongoni mwetu na dunia itakuwa nzuri zaidi.´

Rais Köhler anatarajiwa leo kuhudhuria mkutano wa pili wa mradi aliouanzisha wa Ushirikiano na Afrika.