1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA:Chama tawala chapata ushindi katika uchaguzi wa magavana

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9a

Hali ya wasiwasi imetanda nchini Nigeria huku matokeo ya uchaguzi wa magavana yakitolewa.Chama tawala cha Peoples Democratik PDP kimejinyakulia nafasi 5 katika majimbo yote saba huku chama cha upinzani cha All Nigeria Peoples kikipata nafasi moja na Peoples Progressive Alliance kukita katika upinzani vilevile katika jimbo la kusini la Abia.

Kwa mujibu wa magazeti nchini humo watu 50 walipoteza maisha yao katika ghasia zilizozuka wakati wa kupiga kura.Uchaguzi huo wa magavana unalenga kutathmini uwezo wa tume ya uchaguzi huku uchaguzi wa rais ukisubiriwa kufanyika Aprili 21 wakati muhula wa Rais Obasanjo ukikamilika.

Visa vya kuiba kura vilevile dosari nyingine zinaripotiwa kufanyika katika uchaguzi huo katika eneo la mafuta mengi la kusini.Uchaguzi huo wa rais ni wa kwanza kufanyika kati ya wagombea wawili walio uongozini nchini humo.

Rais Olusegun Obasanjo alikubali kuwa ghasia zilitokea katika baadhi ya maeneo.