ABUJA : Wafanyakazi wa mafuta wa kigeni waachiwa huru | Habari za Ulimwengu | DW | 03.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA : Wafanyakazi wa mafuta wa kigeni waachiwa huru

Wafanyakazi sita wa kigeni waliotekwa kutoka mtambo wa mafuta wa Nigeria unaoendesha na kampuni kubwa kabisa ya nishati ya Marekani ya Chevron hapo tarehe Mosi Mei wote wameachiliwa huru.

Waasi wa kundi la Vuguvugu la Ukombozi wa jimbo la Niger Delta ambao waliwateka nyara wamesema Wataliana wanne, Mmarekani mmoja na Mcroatia mmoja wamekabidhiwa kwa serikali ya jimbo hapo jana.

Kundi hilo la waasi pia limetangaza kwamba litasitisha mashambulizi kwa mitambo ya mafuta kwa mwezi mmoja kutowa nafasi ya kufanyika kwa mazungumzo na serikali.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com