Abuja. Uchaguzi wa rais leo. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Abuja. Uchaguzi wa rais leo.

Saa chache kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa rais nchini Nigeria, mgombea ambaye anagombania nafasi ya makamu wa rais amenusurika kuuwawa kwa risasi katika eneo la Yenagoa katika eneo linalopatikana mafuta kwa wingi nchini humo la delta ya kusini.

Wapiganaji walishambulia makao makuu ya Goodluck Jonathan ambaye anagombea kwa tiketi ya chama tawala cha Peoples Democratic Party PDP.

Katika mji wa Kaduna upande wa kaskazini ya nchi hiyo, vyama vya upinzani vinadai kukamata makaratasi ya kura yaliyokuwa katika gari.

Lakini tume ya uchaguzi nchini Nigeria imesema kuwa uendeaji kinyume uchaguzi hauwezi kutokea kwasababu karatasi mpya za kupigia kura kutoka nje ya nchi bado hazijasambazwa.

Vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa mbili baada ya muda wa kawaida uliopangwa.

Wagombea wanaoongoza ni pamoja na Umaru Yar’Adua wa chama tawala cha PDP na Muhammadu Buhari wa chama cha upinzani cha All Nigeria Peoples Party. Pia anagombea Atiku Abubakar, mgombea ambaye amerejeshwa katika kinyang’anyiro hicho na mahakama kuu nchini Nigeria.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com