ABUJA : Jeshi la Umoja wa Afrika laongezewa muda Dafur | Habari za Ulimwengu | DW | 01.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABUJA : Jeshi la Umoja wa Afrika laongezewa muda Dafur

Habari kutoka Abuja zinasema Umoja wa Afrika umeongeza muda wa vikosi vyake ya kulinda amani huko Dafur nchini Sudan kwa miezi sita zaidi.

Msemaji wa Umoja wa Afrika amesema hakuna makubaliano ya kuongeza kikosi hicho cha wanajeshi 7,000.Rais Omar al Bashir wa Sudan ameondoka katika mkutano wa viongozi huko Abuja kwa mara nyengine akikataa kuongezwa kwa wanajeshi wa kulinda amani Umoja wa Mataifa kwenye kikosi hicho cha Umoja wa Afrika. Bashir amesema Umoja wa Mataifa unapaswa tu kutuma ushauri wa kiufundi na msaada wa kifedha.

Mgogoro wa Dafur umewapotezea makaazi watu milioni mbili na nusu na kuwapotezea maisha watu 200,000.

Mjini Geneva mataifa 29 wanachama wa Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa wameitisha kikao cha dharura juu ya suala la Dafur.

Finland inasema hali ni mbaya sana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com