1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA : Ghasia zatia dosari chaguzi za majimbo

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9t

Ghasia zimetia dosari duru ya kwanza ya chaguzi za wabunge wa majimbo na magavana nchini Nigeria hapo jana.

Ukiukaji wa taratibu za kupiga kura ikiwa ni pamoja na kujaza masanduku ya kura kwa kura bandia ulikuwa dhahiri hususan katika jimbo la kusini lenye kuzalisha mafuta ambapo takriban watu 17 wameuwawa katika ghasia za kisiasa wakiwemo polisi wanane na wanasiasa watatu.

Rais Olesegun Obasanjo bado ana imani kwamba matokeo ya uchaguzi huo yatakuwa halali.

Waangalizi wa masuala ya kisiasa wameripoti kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura hapo jana hailingani kabisa na idadi halisi ya watu wa nchi hiyo.