1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABU DHABI: Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran azuru Umoja wa Milki za Kiarabu

13 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2V

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran amewasili Umoja wa Milki za Kiarabu kwa ziara ya siku mbili.

Rais Mahmoud Ahmadinejad amekuwa rais wa kwanza wa Iran kuwahi kutembelea Umoja wa Milki za Kiarabu, taifa ambalo ni mshirika wa Marekani.

Rais huyo wa Iran alilakiwa na rais wa taifa hilo Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahayan pamoja na maafisa wengine wakuu wa serikali.

Sheikh Khalifa bin Zayed al-Nahayan amesema serikali yake inataka kukabiliana na hali zinazosababisha hali ya wasiwasi katika eneo la Mashariki ya Kati.

Rais wa Iran anatembelea Umoja wa Milki za Kiarabu punde baada ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Dick Cheney, ambaye ziara yake ilishughulikia Iran, taifa linaloendelea kujistawisha kwa kasi katika eneo la Mashariki ya Kati.