ABIDJAN.Mwanadiplomasia wa umoja wa ulaya auwawa | Habari za Ulimwengu | DW | 07.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABIDJAN.Mwanadiplomasia wa umoja wa ulaya auwawa

Mwanadiplomasia wa umoja wa ulaya mwenye asili ya Ufaransa ameuwawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake katika mji mkuu wa Abidjan nchini Ivory Coast.

Msemaji wa ubalozi wa Ufaransa amesema mwanadiplomasia huyo Michel Miaucel alikuwa mkuu wa maswala ya usalama wa umoja wa ulaya.

Uchunguzi umeanzishwa mara moja.

Haijajulikana bado iwapo mauaji hayo yanaambatana na sababu za kisiasa.

Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imegawanyika baina ya waasi wa kaskazini na serikali ya kusini iliyo mamlakani tangu vita vya mwaka 2002 na 2003.

Visa vya ujambazi wa kutumia silaha unaolenga makaazi ya watu mahiri au watalaamu vimeongezeka kwa kasi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com