ABIDJAN: Wanamgambo wamewasilisha silaha Ivory Coast | Habari za Ulimwengu | DW | 20.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABIDJAN: Wanamgambo wamewasilisha silaha Ivory Coast

Wanamgambo walioiunga mkono serikali ya Ivory Coast wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2002 hadi 2003,wamekamilisha operesheni ya kuwasilisha silaha.Katika sherehe ilyohudhuriwa na Rais Laurent Gbagbo,zaidi ya silaha 1,000 ziliwasilishwa kama ishara ya zoezi hilo.Hatua ya kukusanya silaha hizo ni miongoni mwa masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya serikali na waasi waliodhibiti eneo la kaskazini wakati wa vita.Makundi ya wanamgambo,mara nyingi yaliungana na vikosi vya serikali kupigana dhidi ya waasi. Mnamo mwezi wa Machi,mchakato wa amani wa Ivory Coast ulipiga hatua kubwa mbele,baada ya Rais Gbagbo na kiongozi wa waasi,Guillaume Soro kutia saini mkataba wa amani.Gbagbo akamtangaza Soro kama waziri mkuu wa Ivory Coast.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com