ABIDJAN : Kagame ataka muungano dhidi ya wanaopiga vita Waafrika | Habari za Ulimwengu | DW | 06.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ABIDJAN : Kagame ataka muungano dhidi ya wanaopiga vita Waafrika

Rais Paul Kagame wa Rwanda ametowa wito wa kuundwa kwa muungano wa nchi za Kiafrika kupambana na kile alichokiita tabia ya kuyapiga vita mataifa ya Afrika hususan nchini Ufaransa nchi ambayo Rwanda imevunja uhusiano wake wa kibalozi.

Katika mahojiano yaliochapishwa katika magazeti kadhaa ya Ivory Coast hapo jana Kagame amekaririwa akisema kwamba lazima waunde muungano wa kupambana na uadui wowote ule dhidi ya Afrika unaowakabili kama vile Ufaransa na adui mwengine yoyote yule.

Kagame pia ametowa wito wa kuwepo kwa ushirikiano kati ya mataifa ya Afrika kusuluhsiha mizozo yao na kuwataka washirika wao wa kigeni wasiwe mabwana wa kutowa amri bali wawe washirika wa kweli.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com