9 wauawa na bomu Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 18.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

9 wauawa na bomu Iraq

BAQUBA:

Watu wasiopungua 9 wameuawa na wengine 18 kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga lililotokea katika mji wa Baquba nchini Iraq.

Mshambuliaji huyo alimejilipua ndani ya msikiti wa Kishia.Shambulio hili ni la pili la kujitoa mhanga katika kipindi cha siku mbili katika mkoa wa Diyala kaskazini mashariki mwa Baghdad.Pia shambulio hilo limekuja wakati wa matayarisho ya siku ya Ashura inayoadhimishwa leo ijumaa.Siku hii ni muhimu katika kalenda ya waislamu wa Kishia. Mwezi jana mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua katika mtaa huo mmoja na kuwauwa wanachama wa baraza maalum ambalo linapambana dhidi ya magaidi wa al qaida nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com