230 wafa baada ya Lori la mafuta kupinduka na kuripuka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo | Habari za Ulimwengu | DW | 12.09.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

230 wafa baada ya Lori la mafuta kupinduka na kuripuka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Watu wpatao 230 wafa baada ya Lori la mafuta kuripuka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Watu wasiopungua 230 wamekufa baada ya Lori la mafuta kuripuka katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo . Kwa mujibu wa taarifa za jeshi la Umoja wa Mataifa linalolinda amani nchini humo watu wengine wapatao 200 wamejeruhiwa. Inahofiwa idadi ya vifo itaongezeka.

Lori hilo lililotekea Tanzania lilipunduka katika kijiji kimoja cha kusini mwa jimbo la Kivu kutokana na mwendo wa kasi kubwa. Waliokufa ni pamoja na watoto zaidi ya 60 na wanawake 36. Wengi wao walikuwa wanatazama mashindano ya kombe la dunia ndani ya vibanda vyao pembezoni mwa barabara.

Gavana wa jimbo Cisamovo amesema ajali imetokea baada ya Lori ,kupinduka na petroli kuanza kumwagika. Kituo cha Radio kinachofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kimearifu kwamba wakaazi wa kijiji hicho walikimbilia kwenye Lori hilo ili kuiba mafuta wakati liliporipuka.

Gavana Cisamovo amesema walinda amani wa Umoja wa Mataifa pia walikuwa miongoni mwa watu waliokufa walipojaribu kuwazuia watu kufika kwenye gari hilo. Hata hivyo taarifa za Umoja wa Mataifa zilisema baadae kwamba hakuna mtu wa Umoja wa Mataifa aliekufa.

 • Tarehe 12.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12X9W
 • Tarehe 12.09.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/12X9W

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com