Kenya imeanza harakati za maziko ya kitaifa ya rais mstaafu Daniel Arap Moi aliefariki dunia mapema leo. Salam za rambi rambi zinamiminika kutoka sehemu tofauti za dunia. Tumepata nafasi ya kuzungumza na mmoja ya waliowahi kufaidi matunda ya sera za Arap Moi. Lakini pia wakati wa utawala wa Moi kulishuhudiwa baadhi ya Wakenya walioikosoa serikali na kumkosoa kiongozi huyo