1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama lishindwa kuafikiana.

Mtullya, Abdu Said30 Aprili 2008

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeshindwa kuafikiana juu ya mgogoro wa Zimbabwe.

https://p.dw.com/p/DrA0
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moonPicha: AP



Baraza  la Usalama la Umoja  wa Mataifa  limeshindwa  kuafikiana  juu ya azimio kuhusu  mgogoro  wa  Zimbabwe kutokana  na  upinzani  wa  Afrika Kusini iliyohoji kuwa mgogoro  huo ni suala  la ndani ya nchi hiyo

Baraza lilishindwa kufikia  tamko la pamoja  juunya  mgogoro wa  Zimbabwe baada  ya  Afrika Kusini kupinga na kuhoji  kwamba  mgogoro huo ni wa watu wa Zimbabwe .

Wajumbe wa nchi za Ulaya,Marekani na Latin Amerika  walitaka  kupelekwa mjumbe maalum wa Umoja  wa  Mataifa.

Mjumbe  wa  Uingereza aliliambia Baraza hilo kuwa  Zimbabwe  inakabiliwa na mgogoro  mkubwa  usiokuwa na mithili  tokea  nchi hiyo ijikomboe. Mjumbe huyo amesema  watu milioni moja na laki tano sasa  wanategemea msaada  wa  chakula.

Hapo  awali  naibu kiongozi wa  chama cha  upinzani nchini  Zimbabwe   alilitata Baraza  la  Usalama  la Umoja  wa Mataifa lipeleke  mjumbe maalumu nchini  Zimbabwe  kuonesha  kuwa jumuiya  ya kimataifa ina dhamira ya kuwasaidia watu wa  Zimbabwe kutatua masuala ya haki  za  binadamu,mgogoro wa kisiasa na  hali  mbaya ya maisha inayowakabili  watu.

Lakini  baraza la Usalama  limeshindwa kuafikiana  juu ya  hatua ya  kuchukua.

Rais wa  Baraza  hilo amesema  sasa ni juu ya  katibu Mkuu wa Umoja  wa Mataifa  Ban Ki-moon kuamua  juu ya kupeleka mjumbe maalumu au  kupeleka ujumbe  utakaochunguza hali ya nchi hiyo.

Wakati Marekani,Uingereza  na Ufaransa  zinataka  Umoja wa Mataifa upeleke mjumbe  nchini Zimbabwe,Afrika kusini,Urusi ,China  na nchi zingine  zinapinga  wazo  la kuchukua  hatua yoyote  kwa  sasa.

Wakati  huo  huo viongozi wa  vyama vya  upinzani wanataka  matokeo  ya uchaguzi wa rais yatolewe  nchini Zimbabwe.