1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZImbabwe yakandamiza wanaharakati wa upinzani

Isabella Mwagodi19 Machi 2007

Viongozi wanne wa upinzani wamezuiliwa kusafiri ngambo na mmoja wao kupigwa na kujeruhiwa vibaya katika uwanja wa ndege wa Harare. Kadhalika serikali ya Zimbabwe imepiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa muda wa miezi mitatu nchini humo.

https://p.dw.com/p/CB5C
Maandamano ya vyama pinzani jijini Harare.
Maandamano ya vyama pinzani jijini Harare.Picha: AP

Nelson Chamisa,Mmoja wa viongozi wa chama cha upinzani cha movement for democratic change ,akiwa kitandani mwake hospitalini Harare,alieleza waandishi habari kwamba watu wanane walimfuata alipotoka nje ya gari lake,wakampiga mangumi,na alipoanguka chini akawaona wakikimbiliaa kwa magari mawili ambayo hayakuwa na nambarii. Alikuwa safarini kuhudhuria mkutano wa Africa, Caribbean Pacific na Umoja wa Ulaya nchini Ubelgiji.

Madakitari wanasema fuvu lake la kichwa limejeruhiwa vibaya.

Ndiyo hali inayowakumba viongozi wa upinzani nchini Zimbabwe,ambao rais Robert Mugabe amewataja kuwa viongozi magaidi wanaotumiwa na nchi za magahribi kuvuruga Zimbabwe . Lakini kiongozi wa upinzani Morgan Changirai amesema ulagahi wa serikali hautakuwa kizuizi kwao. Kwamba wataendeleas kupigania haki za zaidi ya raia mia tano waliofariki wakingangania uhuru wa kidemokrasia nchini humo.

Hatahivyo Waziri wa habari wa Zimbabwe, Sikanyiso Ndlovu,alikana kuwa serikali ilihusika katika mashambulizi hayo au, inatumia nguvu za kimabavu kudhulumu upande wa upinzani.

Wanaharakati wengine wanaogombania demokrasia nchini Zimbabwe,Grace Kwinje na Sekai Holland walijaribu kwenda Afrika Kusini kupata matibabu zaidi,baada ya kupigwa na mapolisi walipokamatwa wiki iliyopita.Lakini walizuliliwa katika uwanja wa ndege wa Harare kwa madai ya kukosa makaratasi yanayotoka kwa wizara ya afya.

Na mwili wa Gift Tandare,kijana aliyeuwawa mapema mwezi Machi katika mkutano wa vyama pinzani,ulidaiwa kuchukuliwa kwa nguvu na idara ya upelelzi ya serikali na wakauzika bila kibali cha familia yake.

Msemaji wa vyama vya upinzani, Eliphas Mokunoweshure amesema,serikali ilifahamu vyema kuwa,ikiwa wangeliruhusu familia hiyo kumzika wenyewe,viongozi wa upinzani wangepata nafasi ya kufanya mkutano mkubwa katika mazishi yake.

Umoja wa Afrika umetaka serikali ya Zimbabwe kuhemshimu haki za raia wake na kutaka mazungumzo ya kuleta amani,kutatua utata wa kisiasa unaozidi kukithiri nchini Zimbabwe. Lakini tena Umoja huo na jirani ya Zimbabwe,Afrika kusini, na pia Umoja wa Mataifa wamelaumiwa kwa kukaa kimya juu ya suala hilo, hasaa baada ya kiongozi wa upinzani wa chama cha movement for democratic change Morgan Tsvangirai,kupigwa katika mkutano wa hadhara huko Harare.

Rais Mugabe amepuuzilia mbali shinikizo la kuleta demkorasia nchini Zimbabwe na hata kunukuliwa kusema,wakosowaji wake wanaweza kujinyonga. Na uongozi wake wa miaka 27 bila shaka,unazidi kuleta mtafaruku na kusababisha hali tete nchini Zimbabwe