1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani Afrika.

13 Januari 2010

Utawala bora Msumbiji ni sharti la msaada.

https://p.dw.com/p/LUqG
Dirk Niebel, FDP.Picha: dpa

Waziri wa misaada ya maendeleo wa Ujerumani Dirk Niebel, akiwa mjini Maputo,Msumbiji kituo chake cha mwisho cha ziara yake ya Afrika ,adhihirika kuondoa shaka shaka zake alizokuwa nazo kabla ya ziara yake kuwa msaada wa fedha katika bajeti za nchi shirika zinazopokea misaada ya maendeleo si sawa.

Lakini, baada ya kujionea mwenyewe hali ya mambo alipokuwa nchini Ruanda na sasa Msumbiji, nchi mbili zinazojipatia msaada wa fedha katika bajeti zao kama washirika wa Ujerumani na Umoja wa Ulaya, sasa ameondoa shaka shaka zake. Kwani msaada wa bajeti unazilazimisha pande zote mbili kuzungumzia mada muhimu za kimsingi, kama vile utawala bora na demokrasia.Mazungumzo ya aina hiyo ya kukosoana baina ya washirika ni ya manufaa na ni msingi wazi pia katika ushirikiano katika sekta ya misaada ya maendeleo.

Akijivunia kabisa, Bw.Dirk Niebel aliwaambia waandishi habari wakati wa ziara yake hii ya Afrika kuwa, kutokana na onyo kali la serikali ya Ujerumani na nchi-fadhili kwa serikali ya Uganda, kuwa isipitishe sheria kali zaidi kuwaadhibu mashoga, serikali ya Kampala inapanga sasa kutopitisha sheria hiyo. Waziri Niebel amesema,

"Nimefurahi sana kusikia kwanza ni waziri wa uwekezaji wa Uganda kusema kwamba yafaa kuzingatia iwapo sheria kali zaidi kupitia adhabu ya kifo kwa tabia ya ushoga bora isipitishwe.Na ikiwa matamshi hayo kwanza aliotoa waziri yatageuka msimamo wa serikali na wa bunge, yatakuwa mafanikio ya diplomasia ya kimya-kimya."

Lakini hayo hayakuwa tu mafanikio ya diplomasia ya faraghani tu, bali yalitokana pia na maneno makali kabisa na misingi iliobainishwa wazi ifuatwe.Wafadhili wameitishia Uganda kuwa watafikiria upya msaada wao katika mfuko wa matumizi wa serikali ya Uganda.

Hata nchini Msumbiji, kituo chake cha sasa cha ziara yake Bw.Niebel, wafadhili hawridhiki na hali ya kisiasa.Rushwa imesheheni, utawala-bora haupo. Na wakati wa uchaguzi wa Oktoba mwaka jana, chama-tawala cha FRELIMO kilifanya udanganyifu katika utaratibu wa uchaguzi. Vyama vya upinzani havikupewa sauti katika vyombo vya habari vya dola na havikuweza hata kugombea uchaguzi katika wilaya 9 za uchaguzi.Jumuiya ya nchi fadhili 19 ikahisi maji yamezidi unga na haikuweza kuvumilia zaidi:

Kwa njia ya barua ikaanzisha kile kilichoitwa "Mazungumzo wazi ya pande mbili" na kuitaka serikali ya Msumbiji kujieleza. Na iwapo wafadhi watoao misaada na wanaopokea misaada hiyo hawataafikiana, mchango wa wafadhi katika bajeti ya Msumbiji hautatolewa tena. Katika mfuko huo, serikali ya Ujerumani inachangia Euro milioni 15 kwa mwaka.

Kwa hivyo, mazungumzo magumu yanamsubiri waziri huyu wa misaada ya maenedeleo wa Ujerumani katika kituo chake hiki cha mwisho mjini Maputo.

Mwandishi: Ute Schaeffer/Ali,Ramadhan /ZR

Uhariri: Miraji Othman