1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Rais Obama ulaya imezaa matunda gani ?

8 Aprili 2009

Safu za wahariri zinaichambua.

https://p.dw.com/p/HSoI
Barack Obama akilahkiana na vijana.Picha: AP

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo, yamechambua mada mbali mbali nyingi za ndani ya nchi kama vile ufyatuaji mwengine wa risasi uliotokea jana huko Bavaria.Katika maswali ya nje, wahariri wengi walichambua ziara iliomalizika jana ya Rais barack Obama barani ulaya hadi Irak na ilizaa matunda gani ?

KOLNISCHE RUNDSCHAU juu ya ziara ya kwanza ya Obama ulaya tangu kuingia Ikulu,laandika::

"Ikulu ya Marekani, imeridhika na inastahiki kuridhika.Yamkini wakati wa ziara yake hiyo ya ulaya,rais Obama, hakufaulu kutimiza shabaha zake zote alizolenga wakati wa mazungumzo yake na viongozi mbali mbali na hata katika ule mkutano wa kilele,jambo moja ni dhahiri-shahiri:

Amefaulu kubadili heba na hisia kwa nchi yake ya Marekani.Wakati George Bush, mtangulizi wake, kwa nadharia alioitumia aliweza mnamo muda wa miaka 8,kuifanya takriban dunia nzima adui yake,yadhihirika ,Obama mwenye kutabasamu,msomi,mwenye uwezo,mwenye kutia maanani masilahi ya washirika wake,mwenye heba ya kuvutia, amefaulu mnamo muda wa wiki chache tu,kuibadili sura ya Marekani na kuifanya ya kupendeza.Kuongoza kwa kupiga mfano mwema kuliko kwa ujuaji na kuwa tayari kushirikiana na wenzio ni mtindo wa Obama.Lakini maneno yapasa kufuatwa na vitendo."

Ama gazeti la BADISCHE ZEITUNG kutoka Freiburg,laandika:

"Mafanikio ya ziara ya rais Obama hasa ni kumuona kwa hotuba zake na kwa kutega sikio lake amefaulu kuleta imani mpya na uaminifu katika uongozi wa Marekani.Isitoshe, amewapa wenyeji wake hisia kwamba anahitaji msaada wsao tena haraka.Kwa umbali gani matumaini aliotoa yatashawishi siasa za kawaida,ni jambo la kusubiri kuona.Mporomoko unaoweza kutokea ni mkubwa mno kutoka juu.Maadui wsanavizia tu ateleze na matatizo yaliopo si madogo.Lakini tujiulize:lini tulikuwa na hisia kama wakati huu kwamba baada ya dhiki si dhiki,bali faraji."

Likigusia ziara ya ghafula jana ya rais Obama nchini Irak ambako aliahidi kuvimaliza vita vya huko,Neue Osnabruecker Zeitung laandika:

"Mapatano iliofunga Marekani na serikali iliochaguliwa ya Irak enzi za utawala wa George Bush,yanaitisha kuondolewa majeshi ya Marekani nchini Irak mwishoni mwa mwaka 2011.

Obama lakini, kinyume na ahadi zake katika kampeni ya uchaguzi amekubali kuheshimu muda huo.Hadi ifikapo kati ya mwaka ujao askari 90.000 kati ya kikosi kizima cha askari 140.000 wataondoka Irak.Mwito alioutoa Obama kwa viongozi wa Irak kubeba binafsi jukumu zaidi na kuwa tayari zaidi kusikizana ni barabara."

Likitukamilishia mada hii, gazeti la Badische Neuste Nachrichten laandika:

"Marekani inauhitaji ulimwengu wakati huu zaidi kuliko dunia inayoihitaji Marekani.Marekani inaihitaji China kutokana na hazina yake kubwsa ya fedha,inazihitaji nchi za Ulaya ili kuwsa na mkakati wa pamoja kwa vita vya Afghanistan.

Likitugeuzia mada,gazeti la COBURGER TAGBLATT lazungumzia ufyatuaji mwengine wa risasi na bahari ya damu uliozuka tena jana Ujerumani.Laandika:

"Linachomoza tena swali iwapo damu iliomwaika jana haingeweza kuzuwiliwa isimwaike.Ingeweza.Kwani, nini kinachozuwia mbele ya majengo ya serikali au ya umma kuwekwa walinzi kushika zamu na kulinda dhidi ya watumiaji nguvu kama hao ?"