1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZAGREB: Wazimamoto wazingirwa na moto Kroatia

31 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBUH

Wazimamoto 5 wamepoteza maisha yao na wengine 14 wamejeruhiwa baada ya kuzingirwa na moto msituni kwenye kisiwa cha Kornati nchini Kroatia.

Wakati huo huo,wazimamoto nchini Ugiriki wamefanikiwa kudhibiti moto katika sehemu mbali mbali,isipokuwa kwa moto mkubwa unaoendelea kuhatarisha eneo linalozunguka mji wa Karytaina, magharibi ya Peloponnes.Katika hatua ya tahadhari wakazi wa vijiji 13 wamehamishwa kwengine.Moto mingine mikubwa inaendelea kuwaka katika Kisiwa cha Euböa,kaskazini-magharibi ya Ugiriki na kisiwani Kreta.

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani,Franz Josef Jung ameamua kurefusha ujumbe wa wanajeshi wa Ujerumani wanaotoa msaada nchini Ugiriki na vile vile kuongeza idadi ya wasaidizi na vifaa.Hivi sasa Ujerumani imepeleka wanajeshi 68 na helikopta 3 za uchukuzi.