1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Yote namwachia Mungu" - Mansoor Himid

27 Agosti 2013

Hatimaye Mansoor Yussuf Himid, mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki mjini Unguja, amekubali kufanya mazungumzo yake ya kwanza na Idhaa ya Kiswahili ya DW tangu uamuzi wa Chama chake cha Mapinduzi wa kumvua uanachama.

https://p.dw.com/p/19XJw
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania.
Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi nchini Tanzania.Picha: imago/Xinhua

Kwa mujibu wa taarifa ya CCM kwa vyombo vya habari ni kwamba Mansoor amevuliwa uwanachama baada ya kukiuka miiko ya chama hicho tawala nchini Tanzania, hasa kwenye suala la muundo wa Muungano.

Katika mazungumzo haya na Sudi Mnette, kwa mara ya kwanza mwansiasa huyo kijana, ambaye hapo jana Halmashauri Kuu ya CCM ilitangaza kumfukuza chamani, ameeleza baadhi ya yale yaliyo moyoni mwake.

Kusikiliza mahojiano kamili, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Khelef