1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Watawa wa Kibudha waandamana kabla ya ziara ya Gambari jumamosi

1 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Au

Watawa wa kibudha nchini Myanmar hapo jana wamefanya tena maandamano kwa mara ya kwanza tangu utawala wa kijeshi nchini humo kuyavunja kwa kutumia nguvu maandamano ya watetea demokrasia mwezi mmoja uliopita.

Kiasi cha watawa 200 wanasemekana waliiandamana katika mji wa Pakokku kilimita 600 kutoka kaskazini mwa mji mkuu Yangon.Maandamano ya mwezi Septemba ambapo watu zaidi ya kumi waliuwawa pia yalianzia kwenye mji huo wa Pakokku.

Jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifuatilia kwa karibu hali ya mambo katika taifa hilo.Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa katika suala la Myanmar Ibrahim Gambari anatazamiwa kurejea kwa mara nyingine nchini humo hapo jumamosi kuwahimiza watawala wa kijeshi kuanzisha mazungumzo na kiongozi wa upinzani aliyeko kizuizini Aung Sa Suu Kyi.