1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

YANGON : Gambari arudi tena Asia

Mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amewasili nchini Thailand hapo jana kuanzisha upya jitihada za mazungumzo ya usuluhishi wa kisiasa katika nchi jirani ya Myanmar ambapo utawala wa kijeshi nchini humo ulivunja kwa nguvu maadamano ya kutetea demokrasia na kuendelea kuwatia mbaroni wapinzani.

Kabla ya kuwasili kwa Ibrahim Gambari watawala wa kijeshi wa Mnyanmar waliregeza kwa kiasi fulani vikwazo walivyoweka nchini humo baada ya maanadamano makubwa dhidi yao mwezi uliopita kwa kurudisha mawasiliano ya mtandao lakini wakiendelea kuzifunga tovuti za habari za kigeni.

Gambari yuko Asia kuratibu hatua za kuchukuliwa na nchi za Asia kukabiliana na mgogoro wa Myanmar ambapo pia anatazamiwa kuzitembelea Malaysia,Indonesia.Japani ,China na Myanmar yenyewe.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com