1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YALA: Afisa mmoja wa jeshi auwawa kwenye mashambulio ya waasi

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQs

Afisa mmoja wa jeshi ameuwawa mapema leo kusini mwa Thailand wakati bomu lilipolipuka nje ya nyumba yake kufuatia uvamizi wa usiku kucha uliofanywa na waasi.

Mlipuko huo ambao pia umemjeruhi kijana wa umri wa miaka minane, unafuatia usiku wa milipuko, ufyatulianaji wa risasi na mashambulio ya waasi yaliyosababisha vifo vya watu wanne na wengine 49 kujeruhiwa.

Duru za polisi zinasema milipuko 12 imewaua watu wawili na kuwajeruhiwa zaidi ya watu 20 katika jimbo la Yala. Jimbo hilo ni mojawapo ya majimbo yaliyo na idadi kubwa ya waislamu yanayokabiliwa na upinzani mkali yanayopakana na Malaysia.

Katika mkoa wa Narathiwat, mtu mmoja aliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kwenye mashambulio sita ya mabomu.

Zaidi ya watu 1,900 wameuwawa katika eneo hilo tangu mwezi Januari mwaka wa 2004. Ijumaa iliyopita serikali ya Thailand ilitangaza kwamba iko tayari kufanya mazungumzo na waasi wa kusini ikisaidiwa na nchi jirani ya Malaysia.