1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wolfsburg yatwaa ubingwa wa Super Cup

4 Agosti 2015

mabingwa wa kombe la shirikisho nchini Ujerumani , DFB Pokal VFL Wolfsburg wamewakera mabingwa wa Bundesliga Bayern Munich siku ya Jumamosi kwa kuibwaga kwa mikwaju ya penalti

https://p.dw.com/p/1G9GT
DFL-Supercup 2015 VfL Wolfsburg - FC Bayern München
Picha: Reuters/F. Bimmer

Ushindi huo uliwapa Wolfsburg ubingwa wao wa kwanza wa Super Cup nchini Ujerumani, katika uwanja wa Volkswagen Arena mjini Wolfsburg.

mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na mikwaju ya penalti ilipopigwa Wolfsburg ilipitisha mpira mara tano na Bayern ikaambulia mikwaju minne tu.

Mchezo huo hufanyika kabla ya kuanza kwa msimu wa Bundesliga ambao unaanza rasmi tatrehe 14 , ambapo mabingwa Bayern Munich watapambana na Hamburg SV. Ni kipigo cha tatu mfululizo kwa Bayern katika kinyang'anyiro hicho , ambapo Super Cup ndio taji pekee mbayo limekuwa likimchoropoka kocha Pep Guardiola tangu aanze kazi ya kuifunza Bayern miaka mitatu iliyopita.

Mwandishi: Sekione Kitojo dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef