Wito wa wanawake kuwa na madaraka zaidi nchini Tanzania | Matukio ya Kisiasa | DW | 30.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Wito wa wanawake kuwa na madaraka zaidi nchini Tanzania

Wabunge wanawake katika bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wamepewa changamoto kuwa kusimamia hoja zinazotetea maslahi ya wananchi ni muhimu kuliko kuangalia maslahi ya vyama vyao.

Akizungumza na wabunge hao wanaokutana mjini Bagamoyo, waziri mkuu mstaafu na mwanasiasa anayeheshimiwa nchini Tanzania, Jaji Joseph Warioba, alisema kutanguliza maslahi ya wananchi itawajengea umaarufu wabunge wanawake.

Mwandishi wetu Christopher Bhuke amehudhuria mkutan huo na ametutumia ripoti ifuatayo.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com