1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wito kuidhinisha upesi Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya

14 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CbV1

LISBON: Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amezihimiza nchi 27 wanachama katika umoja huo,kuidhinisha upesi Mkataba wa Mageuzi wa Umoja wa Ulaya uliotiwa saini mjini Lisbon. Kuambatana na mpango wa Barroso,mkataba huo uanze kutumika tarehe 1 Januari mwaka 2009.

Mkataba huo unatazamiwa kufungua ukurasa mpya katika historia ya Umoja wa Ulaya na kuimarisha demokrasia katika utaratibu wa kupitisha maamuzi.