WINDHOEK: China na Namibia kuimarisha uhusiano wa kibiashara | Habari za Ulimwengu | DW | 06.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WINDHOEK: China na Namibia kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Rais Hu Jintao wa China akiendelea na ziara yake barani Afrika ametia saini makubaliano ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Namibia yenye utajiri mkubwa wa malighafi.Hata utalii kati ya nchi hizo mbili unatazamiwa kuimarishwa. Rais Hu vile vile ameahidi kuisaidia Namibia kujenga shule nchini humo.Leo,ziara ya Hu inampeleka Afrika ya Kusini,ambayo kibiashara barani Afrika,ni mshirika mkuu wa China.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com