1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WikiLeaks yatoa nyaraka za siri

29 Novemba 2010

Ni nyaraka ambazo zinaifedhehesha Marekani, na huenda zikaharibu uhusiano wake na washirika wake. Nyaraka hizo ni mawasiliano yaliyonukuliwa kati ya wanadiplomasia wa Marekani na Washington.

https://p.dw.com/p/QKcq
Nyaraka za siri za WikiLeaks zawakosoa viongozi kadhaa duniani, akiwemo Kansela Angela Merkel.Picha: picture-alliance/dpa

Mtandao wa WikiLeaks umetoa maelfu ya nyaraka za siri zinazofichua mawasiliano kati ya Marekani na balozi zake duniani. Nyaraka hizo zimechapishwa na jarida la The New York Times, The Guradian na gazeti la Der Spiegel la hapa Ujerumani. Ikulu ya Marekani mara moja iliitaja hatua hiyo kuwa hatari na isiyowajibika. WikiLeaks ilizitoa nyaraka hizo kwa magazeti hayo licha ya onyo kutoka maafisa wa Marekani kwamba kufichuliwa kwa taarifa hizo kutayaweka maisha ya watu hatarini na itakuwa ni kinyume cha sheria. Nyaraka hizo za siri zinafichua matamshi ya mabalozi kuwakosoa viongozi kadhaa duniani.Pia kuna taarifa ya sisitizo kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabia kuitaka Marekani kuishambulia kijeshi Iran. Tarifa nyingine inasema Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton aliwaagiza wanadiplomasia katika Umoja wa Mataifa kuwapeleleza wanadiplomasia wa kigeni, kwa kukusanya taarifa kuwahusu kama vile email zao za siri, taratibu zao za kufanya kazi pamoja na maelezo ya kadi zao za pesa.