1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wiesbaden:Ujerumani

15 Oktoba 2007

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na rais Vladimir Putin wa Urusi leo wameendelea na mazungumzo yao mjini Wiesbaden magharibi mwa Ujerumani

https://p.dw.com/p/C77m
Kansela Merkel wa Ujerumani na rais Putin wa Urusi
Kansela Merkel wa Ujerumani na rais Putin wa UrusiPicha: picture-alliance/dpa

Viongozi hao wamejadili mpango wa Marekani wa kuweka ulinzi dhidi ya makombora katika Ulaya ya mashariki pamoja na suala la uhuru wa Kosovo.Kansela Merkel na rais Putin pia wamezungumzia juu ya mgogoro wa nyuklia wa Iran.

Wakati huo huo katika mahojiano na gazeti la Die Welt,kansela Merkel amesema Iran inaweza kuwekewa vikwazo madhubuti ikiwa haitaacha mpango wake wa nyuklia.Hatahivyo ameeleza kuwa mgogoro huo unaweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Amesema Iran ni tishio siyo tu kwa Israel bali pia kwa eneo lote la mashariki ya kati,Ulaya na dunia nzima.

Kwenye mazungumzo yao mjini Wiesbaden wajumbe wa Urusi na Ujerumani pia watazingatia masuala yanayohusu matatizo na uhusiano baina ya nchi zao mbili.

Kensela Merkel amesema atatumia fursa ya mkutano wa leo kupeana mawazo kwa ukamilifu na rais Putin.