1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WHO yakutana kwa dharura kuhusu kirusi kipya cha corona

Saleh Mwanamilongo
22 Desemba 2020

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, linakutana kwa dharura katika juhudi za kupambana na kuenea kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, huku mataifa ya Ulaya yakitarajiwa kuanza chanjo dhidi ya Covid-19 ifikapo Jumapili ijayo.

https://p.dw.com/p/3n6jE
Südafrika Corona-Pandemie Johannesburg
Picha: Luca Sola/Getty Images/AFP

Hans Kluge, mkuu wa shirika la WHO kwenye nchi za Ulaya, amesema ni lazima kupunguza safari ili kupambana na kuenea kwa kirusi kipya cha Corona hadi taarifa zaidi itakapotolewa. Lakini Kluge amesema kusafirishwa kwa bidhaa muhimu kunawezekana.
Shirika la WHO lilitahadharisha kuhusu dhana kwamba kirusi hicho kipya, likiwesema ni sehemu ya kawaida ya janga hili la corona na kuipongeza Uingereza katika ugunduzi wa kirusi hicho.

Kwenye taarifa yake, WHO imesisitiza kwamba hakujakuweko na taarifa zaidi ili kufahamu ikiwa chanjo itakuwa na nguvu dhidi ya aina hiyo mpya ya kirusi cha corona. Uingereza imeendelea na juhudi zake za kupunguza maambukizo ya corona huku nchi kadhaa zikisitisha safari zake nchini humo. Hali hiyo imejiri huku siku chache kabla ya kutekelezwa kwa mkataba wa Brexit.

Malori yanayobeba mizigo kutoka Uingereza yalizuiliwa kutoingia katika nchini nyingine za Ulaya. Waziri mkuu wa Uingereza, Boris Johnson aliwasiliana na Rais Emamanuel Macron wa Ufaransa kwa ajili ya kuruhusu malori kuingia nchini humo, kwenye kipidi hiki cha Krismasi. Johnson na washauri wake wanasema kwamba aina mpya ya kirusi cha corona, ambacho kinaaminika kinaambukiza kwa asilimia 70, kiligundulika kwa sababu wanasayansi wa Uingereza wako makini katika uchunguzi wa kirusi hicho.

Großbritannien Folkestone | Grenzschließung Frankreich | Verkehr in
Malori ya Uingereza yaliyokwama mpakani mwa UfaransaPicha: Kirsty Wigglesworth/AP Photo/picture alliance

Shirika la utangazaji la Uingereza, BBC, kilisikika kikielezea kwamba waziri wa Ufaransa wa maswala ya Ulaya, Clement Beaune, alisema kwamba nchi yake inatarajiwa kufikiwa makubaliano ya kuanzishwa upya biashara na Uingereza ifikapo Jumatano.
Kampuni ya Ujerumani ya BioNtech iliyoendesha uchunguzi wa chanjo yake iliyotengenezwa kwa pamoja na kampuni ya Marekani ya Pfizer dhidi ya virusi vya Corona inatarajiwa kusafirisha chanjo milioni 12.5 kwenye nchi za Umoja wa Ulaya kabla ya mwaka huu kumalizika. Hapo Jumatatu, kituo cha kuchungaza madawa cha Umoja wa Ulaya kilitoa ridhaa kwa ajili ya matumizi ya chanjo hiyo.
 

Waziri wa Afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema waatalamu wa Ulaya wamesema aina mpya ya kirusi haitoathiri nguvu ya chanjo ya corona iliyopo kwa sasa. Huku hayo yakiarifiwa, wabunge wa Marekani wamekubaliana kutoa kitita cha dola bilioni 900 zitakazowasaidia Wamarekani walioathirika na virusi vya corona. Fedha hizo pia zitatumika kusambaza chanjo ya corona kote nchini humo na kusaidia katika masuala ya fedha. Bunge la Congress linatarajiwa kuidhinisha mpango katika taifa hilo lililo na idadi ya juu kabisa ya vifo vitokanavyo na Covid-19 ulimwenguni.