1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Westerwelle aungwa mkono na FDP

31 Agosti 2011

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle anaendelea kukosolewa, licha ya kuungwa mkono na viongozi wa chama chake cha FDP wanaokutana kwa kikao maalum nje ya jiji la Cologne.

https://p.dw.com/p/Rj3k
Der Bundesvorsitzende der FDP, Aussenminister Guido Westerwelle, blickt am Freitag (13.05.11) in der HanseMesse in Rostock bei seiner Rede auf dem Bundesparteitag der FDP nach unten. Bei dem Parteitag sollen wichtige Antraege zur Energiewende, zur Bildungs- und zur Europapolitik verabschiedet werden. Zudem soll die Parteispitze insgesamt neu aufgestellt werden. (zu dapd-Text) Foto: Clemens Bilan/dapd
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido WesterwellePicha: dapd

Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha SPD Andrea Nahles, amesema, Westerwelle hajidhuru yeye binafsi tu, bali hata chama chake na serikali ya mseto ya Ujerumani. Ameliambia gazeti la Morgen Post, sera za waziri wa nje Guido Westerwelle, zinachafua taswira ya Ujerumani. Mwanasiasa huyo wa SPD akiwakosoa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wa chama cha CDU na makamu wake Philipp Roesler wa FDP, alisema wakimuachia Westerwelle kuendelea kuvuruga mambo, basi wanasiasa hao wanayatanguliza maslahi yao binafsi na sio ya taifa la Ujerumani.

Hapo jana, Phillip Roesler,alie pia mwenyekiti wa FDP, alisema mdahalo kuhusu kujiuzulu kwa Westerwelle umemalizika. Viongozi wa chama hicho wanamuunga mkono waziri wa mambo ya nje wa hivi sasa Westerwelle. Na hata katika siku zijazo hilo halitobadilika alisisitiza Roesler alipozungumza kwenye mkutano wa viongozi na wabunge wa FDP huko Bergisch Gladbach.

Caption Christian Lindner, Generalsekretär der FDP, aufgenommen am 27.03.2011 während der ARD-Talksendung "Anne Will" zum Thema: "Der Schwabenstreich - Schicksalswahl für Merkel?" in den Studios Berlin-Adlershof. Foto: Karlheinz Schindler
Katibu Mkuu wa chama cha FDP, Christian LindnerPicha: picture alliance/dpa

Hata Katibu Mkuu wa chama cha FDP, Christian Lindner akijaribu kuumaliza mdahalo huo, alisema, Westerwelle ametekeleza miradi muhimu na anaungwa mkono kwa hayo yote, alisisitiza Lindner. Amesema,mdahalo huo kuhusu Westerwelle, kwa sehemu kubwa unachochewa na wanasiasa wa upinzani. Uvumi kuwa Westerwelle atatimuliwa ikiwa chama cha FDP kitashindwa katika chaguzi mbili zijazo majimboni, ni dhana zisizo na msingi.

Sigmar Gabriel, chairman of the German Social Democratic Party, (SPD, speaks during a party meeting in Berlin, Germany, Sunday, Sept. 26, 2010. (AP Photo/Michael Sohn)
Mwenyekiti wa chama cha SPD, Sigmar GabrielPicha: AP

Kwa upande mwingine, mwenyekiti wa chama cha SPD, Sigmar Gabriel amemtaka Kansela Merkel kuchukua hatua. Amesema,Kansela hawezi kuiachilia Ujerumani kupoteza uaminifu wake katika nchi za nje. Akasisitiza kuwa Kansela anawajibika kwa makosa yote yaliyofanywa na waziri wa nje Westerwelle. Amesema, sasa ni lazima kwa serikali kuwa tena na sera za nje zinazoaminika.

Waziri Westerwelle alianza kulaumiwa vikali, alipozuia kura ya Ujerumani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kuunga mkono operesheni ya jumuiya ya kujihami ya NATO nchini Libya mnamo mwezi wa Machi mwaka huu. Na hivi karibuni badala ya kuisifu waziwazi operesheni ya NATO alisema, sera ya kuiwekea vikwazo Libya ndiyo iliyosaidia kuuangusha utawala wa Muammar Gaddafi. Baadaye alikiri hadharani kuwa Walibya ndio walioipindua serikali ya Gaddafi kwa msaada wa NATO.

Kwa maoni ya viongozi na wabunge wa FDP wanaokutana Bergisch Gladbach mdahalo wa Westerwelle umemalizika. Mkutano wao sasa unashughulikia mpango wa kuiokoa sarafu ya Euro, sera za kiuchumi katika masoko ya dunia, haki za raia, na elimu.

Mwandishi: Martin, Prema/dpa

Mhariri: Josephat Charo