1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates azuru Irak

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5fQ

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates, amekutana na makamda wakuu wa jeshi la Marekani mjini Baghdad hii leo.

Waziri Gates amejadili kasi ya kuwapunguza wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak, siku moja baada ya wanamgambo kuwaua watu zaidi ya 50 katika wimbi la mashambulio.

Robert Gates amesema licha ya machafuko kupungua nchini Irak katika miezi michache iliyopita, hali ya usalama nchini humo bado inatia wasiwasi.

Waziri Gates amemsifu luteni kanali Ray Odierno, naibu kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak, kwenye sherehe ya kuwapa nishani wanajeshi wa Marekani mjini Baghdad hii leo.

Odierno anaondoka Irak baada ya kuyasimamia makao makuu yanayoongoza juhudi za kutekeleza mpango wa kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak, David Patraeus, kila siku.

Odierno anarejea mjini Washington na ameteuliwa na rais George W Bush apandishwe cheo na kuwa naibu wa mnadhimu mkuu wa jeshi la Marekani.