1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani ziarani kanda ya Balkan

26 Agosti 2010

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle hii leo anaendelea na ziara yake katika kanda ya Balkan kwa kuzitembelea Serbia na Bosnia.

https://p.dw.com/p/OweU
Außenminister Guido Westerwelle (FDP) spricht am Mittwoch (25.08.2010) auf dem Flug nach Zagreb mit Journalisten. Westerwelle ist zu einer dreitägigen Balkan-Reise aufgebrochen. Foto: Hannibal dpa/lbn +++(c) dpa - Bildfunk+++
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Guido Westerwelle.Picha: picture alliance/dpa

Mada kuu ya majadiliano yake katika mji mkuu wa Serbia Belgrade,ni mgogoro unaohusika na suala la kuutambua uhuru wa Kosovo.

Majadiliano yanayohusika na uanachama wa Serbia katika Umoja wa Ulaya, hayakufanikiwa mpaka hivi sasa kwa sababu ya nchi hiyo kukataa kutambua uhuru wa Bosnia. Hii leo mjini Belgrade, waziri Westerwelle atakutana na Rais Boris Tadic na maafisa wengine wa Serbia.

Westerwelle alianzia ziara yake nchini Croatia na aliarifu kuwa nchi hiyo inakaribia kukamilisha utaratibu wa kuingia katika Umoja wa Ulaya.

Mhariri: P.Martin/ZPR