1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya utatanishi.

Abdu Said Mtullya7 Mei 2009

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman afanya ziara nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/Hlad
Waziri wa mambo ya nje wa Israel Avigdor Lieberman.Picha: AP

Waziri  wa  mambo  ya nje wa Israel Avigdor Liebermann  leo  ameanza ziara nchini  Ujerumani  kituo  cha  mwisho katika ziara  yake barani  Ulaya.

Waziri Lieberman  ambae  ni kiongozi wa chama  chenye  mrengo mkali wa kizalendo  nchini  Isreal- Beiteinu aliwasili  mapema  leo  mjini Berlin na amekutana na  wajumbe  wa kamati  ya bunge  la  Ujerumani  inayoshuhgulikia masuala  ya  mambo ya  nje.

Waziri Lieberman amewasili nchini Ujerumani  baada  ya kuzuru,Italia, Ufaransa,Umoja  wa  Ulaya  na Jamhuri ya Czech.

Waziri  huyo  kwa  mara  nyingine amepinga suluhisho la nchi mbili badala yake amezungumzia  alichoita  kiwanda cha amani ambacho  hadi  leo  hakijazaa matunda  bali kimesababisha  fedha zipotee.

Hatahivyo  baada ya mazungumzo  yake na  wajumbe  wa kamati ya masuala ya nje  ya  bunge  la Ujerumani  mjini Berlin, anatarajiwa  kukutana  na waziri wa  mambo  ya nje  wa  Ujerumani Frank Walter Steinmeier  na  waziri  wa mambo  ya ndani  Wolfgang Schauble.

Hapo  awali   mwanasiasa  huyo  wa Israel  alitembelea  kumbukumbu  ya maangamizi  ya  wayahudi mjini  Berlin.

Mwandishi :A.Mtullya /AFPE   

Mhariri:M.Abdul-Rahman