1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Urussi Putin asema haamini Iran inatengeneza Bomu

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAOe

PARIS

Waziri mkuu wa Urussi Vladmir Putin amenukuliwa kusema kwamba haamini Iran inataka kutengeneza sialaha za Nuklia.Msimamo huo wa Putin unatofautiana na ule wa Marekani na viongozi wengine wa jumuiya ya kimataifa ambao wanahofia mpango wa kinuklia wa Iran unaazimia kutengeneza silaha za maangamizi.Matamshi hayo ya Urussi yamekuja wakati bodi ya magavana ya shirika la kimataifa la kudhibiti technologia ya Nuklia IAEA imepanga kukutana jumatatu katika kikao maalum ambacho kinatazamiwa kugubikwa na mjadala kuhusu ripoti inayoeleza juu ya kukataa kwa Iran kuweka wazi shughuli zake za kinuklia.

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya mkuu wa shirika hilo la IAEA Mohammed Albaradei,Iran bado inatakiwa kutoa maelezo kamili yatakayounga mkono hoja yake kwamba mradi wake wa Kinuklia haulengi kutengeneza bomu la Nuklia kama inavyodaiwa na nchi za magharibi.

Aidha ripoti hiyo inasema kwamba Iran inaendelea na shughuli zake za kurutubisha madini ya Uranium licha ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa kuitaka nchi hiyo kukomesha mpango wake huo.