1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Uingereza ziarani India

20 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cv5q

NEW DELHI: Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown amewasili nchini India kwa ziara ya siku mbili.Amesema, anatazamia kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo mbili katika sekta za uchumi,utamaduni na elimu.Matumaini yake ni kuwa Uingereza na India zitashirikiana zaidi kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupiga vita ugaidi kote duniani.Waziri Mkuu Brown ametokea China ambako pia mada kuu zilihusika na uchumi na njia za kupunguza uchafuzi wa mazingira.