Waziri mkuu wa Ivory Coa´st amenusurika na jaribio la kutaka kumuuwa | Habari za Ulimwengu | DW | 30.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Waziri mkuu wa Ivory Coa´st amenusurika na jaribio la kutaka kumuuwa

Bouake:

Waziri mkuu wa Ivory Coast Guillaume Soro amenusurika na shambulio la kombora dhidi ya ndege aliyokua akisafiria.Abiria wasiopungua wanne wa ndege hiyo wameuwawa.Makombora matatu na risasi zilifyetuliwa ndege aliyokua akisafiria waziri mkuu Guillaume Soro ilipokua ikitua Bouake-mkao makuu ya chama chake cha Forces Nouvelles.Chama hicho kilikua kikilidhibiti eneo la kaskazini la Ivory Coast tangu waliposhindwa kumpindua rais Laurent Gbagbo mwaka 2002.Waziri mkuu Guillaume Soro alikwenda Bouake kusherehekea kutiwa njiani mfumo mpya wa sheria-tukio linaloangaliwa kua muhimu katika kuimarisha utaratibu wa amani uliolengwa kuiunganisha Ivory Coast.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com