1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Israel ahojiwa tena na polisi kuhusu madai ya rushwa

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E53B

JERUSALEM

Polisi nchini Israel wamemuhoji kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki mbili waziri mkuu Ehud Olmert kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yake.Wizara ya sheria nchini humo imefahamisha kwamba uchunguzi huo unafanywa kuhusu madai ya kuhusika na visa vya rushwa dhidi ya waziri mkuu Olmert katika kipindi kabla ya kuchukua wadhifa huo.

Polisi wanamshuku Olmert kwa kupokea kinyume na sheria dolla nusu millioni kutoka kwa mfanyibiashara mmoja Mmarekani mwenye asili ya kiyahudi Morris Talansky.

Mfanyibiashara huyo anatazamiwa kutoa ushahidi wake jumanne.Waziri mkuu Olmert ambaye alikuwa Meya wa mji wa Jerusalem wakati huo amekiri kupokea michango kwa ajili ya kusimamia Kampeini zake lakini amekanusha kwamba amewahi kupokea hongo.Ametishia kujiuzulu ikiwa waendesha mashtaka watatoa ushahidi wa kutosha kumuhusisha na rushwa.