1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mku Foaud Siniora ajitahidi kumaliza hali ya wasiwasi

24 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSl0

Waziri mkuu wa Lebanon, Fouad Siniora, leo amejitahidi kutuliza wasiwasi mkubwa unaozidi kufuatia kuondoka madarakani rais Emile Lahoud. Sioniora ameahidi atafanya kila awezalo kuhakikisha Lebanon inapata rais mpya haraka iwezekanavyo.

Katika matamshi yake ya kwanza tangu rais Lahoud alipoondoka ikulu bila mrithi, waziri mkuu Fouad Siniora ameitetea serikali yake akisema itaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa katiba.

Siniora ameyasema hayo baada ya kukutana hii leo na Nasrallah Sfeir, kiongozi wa kanisa la kikatoliki la Maronite lenye ushawishi nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa katiba wadhifa wa rais wa Lebanon umetengewa kanisa hilo na wapatanishi walijaribu kushauriana na Nasrallah Sfeir asaidie kumtafuta mtu atakayefaa kuwa rais atakayekubalika na pande zote husika nchini Lebanon.

Makundi hasimu yanayoiunga mkono na kuipinga Syria yatakutana tarehe 30 mwezi huu kumchagua rais mpya atakayechukua mahala pa rais aliyeondoka, Emile Lahoud.