1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wawili wauawa Gaza

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Ce9a

GAZA.Vikosi vya Israel vikiwa na vifaru hii leo vimevamia eneo la Ukanda wa Gaza na kuwaua wapiganaji wawili wa kipalestina.

Maafisa wa kijeshi wa Palestina wamesema kuwa vikosi hivyo vilivyoko kwenye eneo la mashariki katika kambi ya wakimbizi ya Maghazi mita chache kutoka uzio wa Gaza, viliwashambulia wapalestina waliyokuwa na bunduki ambapo wawili kati yao waliuawa.

Kundi la wanamgambo wa Islamic Jihad limedai kuwa waliyouawa ni wapiganaji wao.

Msemaji wa jeshi la Israel alithibitsha kufanyika kwa shambulizi hilo akisema kuwa ni muendelezo wa harakati za kupambana na vitisho vya ugaidi.