1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wavulana 547 wadhalilishwa shule ya kwaya Ujerumani

Admin.WagnerD18 Julai 2017

Takriban watoto wa kiume 547 katika shule ya kwaya ya Wakatoliki Ujerumani waliteswa kingono au kukabiliwa na matumizi mengine ya nguvu kwa kile wahanga walichokilinganisha na "gereza, motoni au kambi  ya mateso".

https://p.dw.com/p/2gkgg
Deutschland Abschlussbericht zu Missbrauchskandal bei Regensburger Domspatzen
Picha: picture alliance/dpa/A. Weigel

"Asasi hii imeelezewa na wahanga kama ni gereza,kuzimu au kambi ya mateso." hayo yametamkwa na wakili Ulrich WeberJumanne (18,07.2017) aliyepewa mamlaka na Kanisa Katoliki wakati akitangaza ripoti ya kurasa 450 ya uchunguzi wa udhalilishaji wa kingono na matumizi ya nguvu ya watoto katika shule mashuhuri ya kwaya ya kanisa ya Regensburger Domspatzen.

Kwaya hiyo ya kanisa ambapo kwa Kiswahili inaweza kuitwa Kasuku wa Kanisa iliodumu kwa mika 1,000 katika jimbo la kusini la Bavaria, hapo mwaka 2010 ilitumbukizwa kwenye kashfa kubwa ya udhalilishaji wa kingono na kuwaharibu watoto kulikumba Kanisa Katoliki duniani.
 

Wahanga wengi wanakumbuka kipindi cha maisha yao katika kwaya hiyo mashuhuri katika mji wa Regensburg kilikuwa kibaya kabisa katika uhai wao kwa kugubikwa na hofu, matumizi ya nguvu na hali ya kukata tamaa, amesema hayo Ulrich Weber ambaye amekabidhiwa na dayosisi miaka miwili iliopita kuchunguza visa hivyo.

Madhila ya ngono na matumizi ya nguvu

Deutschland Abschlussbericht zu Missbrauchskandal bei Regensburger Domspatzen
Ulrich Weber akiwasilisha repoti yake.Picha: picture alliance/dpa/A. Weigel

Akiwasilisha ripoti yake ya mwisho kuhusu dhuluma zilizotokea baina ya mwaka 1945 na mapema miaka ya 1990, Weber amesema amegunduwa matukio 67 ya madhila ya kingono na 500 mengine ya matumizi ya nguvu mwilini ambapo baadhi ya watoto walikuwa wahanga wa matukio yote mawili.
 

Idadi hiyo ni zaidi ya maradufu ya kesi  231 za dhuluma zilizoripotiwa kufanywa na wachungaji wa kanisa hilo na walimu, Weber amegunduwa kupitia mahojiano kufikia mwezi wa Januari mwaka 2016 wakati aliposema wahanga walizungumzia ubakaji, mashambulio ya  ngono, kupigwa vibaya na kunyimwa chakula.

Utamaduni wa kukaa  kimya

Deutschland Regensburger Domspatzen
Watoto wakiwa katika kwaya za kanisa.Picha: picture alliance/dpa/J. Woitas

Weber ambaye hakuweza kuzungumza na wanfunzi wote wa zamani wa shule hiyo amesema anakadiria idadi hiyo ya wahanga kuwa kama 700.

Ametaja utamaduni wa kunyamaza kimya ambao umekusudia kulinda sifa ya kwaya hiyo mashuhuri ya wavulana na vijana wadogo ambayo ina rikodi nyingi na imefanya maonyesho yake duniani kote.
 

Kutokana na hali hiyo amemtwisha lawama kwa kiasi fulani mkuu wa zamani wa kwaya hiyo ya shule, Georg Ratzinger, ambaye ni kaka mkubwa wa papa wa zamani Benedict wa 16.
 

Mwandishi: Mohamed Dahman/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef