1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waumini wasulubiwa Ufilipino

21 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DSIg

CUTUD-UFILIPINO:

Takriban watu 20,mkiwemo kijana wa umri wa miaka 15,wamesulubiwa msalabani na wengine wengi kujiumiza migongo yao kwa kuuiipiga hadi kuvuja damu katika kitendo cha kuikumbuka siku ya leo ya Ijumaa kuu ambayo inaashiria kifo cha Yesu.

Kujitolea kusulubiwa katika maeneo ya kaskazini mwa ufilipino ndio lama ya juu ya kuonyesha imani ya kidini katika taifa lenye wakristo wengi. Katika nchi hiyo wakristo mamilioni kadhaa hushinda wakifunga na kusali wakijiandaa kwa likizo ya Pasaka ambayo imeanza leo.