1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wengine 2 wafariki kutokana na Ebola DRC

Caro Robi
22 Mei 2018

Watu wengine wawili wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

https://p.dw.com/p/2y6Jj
Kongo Ebola Sicherheitsmaßnahmen in Mbandaka
Picha: Reuters/K. Katombe

Wizara ya afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeripoti vifo viwili zaidi vilivyosababishwa na maambukizi ya ugonjwa Ebola. Kulingana na taarifa zinazotolewa kila siku na wizara hiyo ya afya kuhusu Ebola, Mtu mmoja amefariki dunia katika mji mkuu wa jimbo la Mbandaka.

Mhudumu mmoja wa afya pia amefariki dunia katika kijiji cha Bikoro ambako mlipuko huo wa virusi vya Ebola uliripotiwa kwanza, mapema mwezi huu. Visa vingine saba vya maambukizi ya Ebola pia vimethibitishwa nchini humo.

Jana wizara hiyo ya afya ya Congo kwa ushirikiano na shirika la afya duniani WHO lilianzisha kampeini kubwa ya kutoa chanjo dhidi ya Ebola mjini Mbandaka.Idadi ya watu waliokufa kutokana na virusi hivyo sasa imefikia 28.