1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanne wauwawa Ivory Coast kwenye machafuko baada ya uchaguzi

2 Desemba 2010

Matokeo kamili rasmi ya uchaguzi yanasubiriwa kutangazwa Ivory Coast

https://p.dw.com/p/QOJP
Laurent Gbagbo, rais wa Ivory Caost anayeondoka madarakaniPicha: picture alliance/PANAPRESS/MAXPPP

Wahalifu waliojihami kwa bunduki wamewaua kiasi ya watu wanane walipowashambulia wafuasi wa mgombea wa urais wa upinzani wa Ivory Coast Alassane Ouattara wakati ambapo matokeo kamili yanasubiriwa. Ghasia hizo zimezuka wakati ambapo rais Laurent Gbagbo anayewania muhula mwengine analaumiana na mpinzani wake mkuu Alassane Ouattara kwa kuhusika na hila, katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia purukushani hizo kwenye wilaya ya Yopougon ya Abidjan, wahalifu waliojihami kwa bunduki waliivamia afisi ya makao makuu ya chama cha RDR cha Ouattara.Eneo hilo ndilo ngome ya upinzani. Kiasi ya watu 50 wanaripotiwa kuwa walikuwamo afisini humo wakisubiri kutangazwa mshindi. Tayari muda wa mwisho wa kuyatangaza rasmi matokeo hayo umepita na viongozi kadhaa duniani wametoa wito kuwataka viongozi wa Ivory Coast kuutatua mkwamo huo wa kisiasa.