Nchini Tanzania katika mkoa wa Tabora, watoto wapatao 19 wamefariki hapo jana kutokana na msongamano kwenye ukumbi wa disco wakati walipokuwa kwenye shamrashamra za sikukuu ya Eid el fitri.
Watoto hao walikuwa na umri kati ya miaka 12 na 17, ambapo wengine kadhaa wamejeruhiwa wawili kati yao wakiwa katika hali mbaya.
Hilo ni tukio baya kabisa kuwahi kutokea wakati wa kipindi cha sherehe za sikukuu hiyo ya Eid el Fitr katika historia ya Tanzania.
Ili kufahamu zaidi juu ya tukio hilo Aboubakary Liongo amezungumza na Mkuu wa Mkoa huo wa Tabora Abeid Mwinyimusa.