1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watibet wawe na uhuru wa usemi na haki ya kuandamana kwa amani

15 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DOsd

BRUSSELS:

Umoja wa Ulaya umetoa wito kwa China ijizuie kutumia nguvu dhidi ya waandamaniji wa Tibet.Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier amesema, viongozi wa Umoja wa Ulaya mkutanoni mjini Brussels, wametoa mwito pia kwa serikali ya China na wawakilishi wa Tibet kujaribu kuwa na majadiliano na kuumaliza mgogoro huo kwa njia amani.

Wakati huo huo,Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalotetea Haki za Binadamu,Louise Arbour ameitaka serikali ya China iwaruhusu Watibet uhuru wa usemi na kuandamana kwa amani.

Huu ni uasi mkubwa kabisa wa kisiasa kutokea Tibet tangu miaka 20.Ghasia hizo zinatokea wakati China ikjitayarisha kwa Michezo ya Olimpiki mnamo mwezi Agosti.