1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wateka nyara wa ndege ya kituruki wamesalim amri

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXy

“Tume ya pamoja ya Umoja wa mataifa na umoja wa Afrika inabidi iingilie kati haraka” –wanasemas hayo wakaazi wengi wa darfour waliolazimika kuyahama maskani yao ili kuyanusuru maisha yao.Wengi wao wanaamini pekee kikosi hicho cha pamoja ndicho kitakachoweza kulinda amani na kudhamini kurejea kwao majumbani mwao.”Hakutakua na amani bila ya wanajeshi wa kimataifa” amesema hayo Ahmed Hirs a naeishi katika kambi ya wakimbizi ya Otash,kaskazini mwa mji wa Nyala.Katika kambi hiyo wanaishi waakimbizi 62 elfu wemngine waliokimbia mauwaji,ubakaji na uporaji.Kikosi cha pamoja na Umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika kitakachokua na wanajeshi 26 elfu,kinatazamiwa kupelekwa Darfour mwakani.Wakimbizi wanalalamika wakihoji huo ni muda mrefu mno.

Ankara:

Watu wawili walioiteka nyara ndege ya shirika laAtlas Jet la Uturuki-na kuilazimisha ituwe kusini mwa nchi hiyo,wamesalim amri.Watu hao wawili wanaodai kua wanachama wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaida,waliiteka nyara ndege hiyo muda mfupi baada ya kuondoka Cyprus ya kaskazini ikiwa na abiria 136 na watumishi sita.Walitaka ndege hiyo ikatuwe Iran au Syria. Ndege hiyo lakini ilituwa Antalya,kusini mwa Uturuki na wengi wa abiria na marubani wakafanikiwa kutoroka.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki , wateka nyara hao ni raia mmoja wa kituruki na mpalastina aliyekua na paspoti ya Syria.Sababu ya kuiteka nyara ndege hiyo haijulikani.