1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasoshalisti washinda uchaguzi Uhispania

10 Machi 2008

Chama cha Kisoshalisti cha Waziri Mkuu wa Uhispania Jopse Luis Rodrigues Zapatero kimejipatia ushindi wa uhakika katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana lakini kimeshindwa kujipatia wingi mkubwa wa viti bungeni.

https://p.dw.com/p/DLXg

MADRID

Zapatero ameuambia umati mkubwa uliokuwa umeemewa kwa furaha kwamba serikali itafunguwa awamu mpya bila ya mvutano na upinzani wa kihafidhina ambao ulikuwa na sauti bungeni.

Zapatero ameahidi kuongoza kwa kuwafilkiria kabla ya mtu yoyote yule wale watu wasiokuwa na kitu chochote.

Wasoshalisti wamejipatia asilimia 44 ya kura na viti 169 katika bunge lenye viti 350 ikiwa imejiongezea viti kutoka 164 walivyokuwa navyo hapo mwaka 2004 wakati takriban asilimia 99 ya kura zikiwa tayari zimehesabiwa.