Wasomali waukimbia Mogadishu | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Wasomali waukimbia Mogadishu

MOGADISHU:

Mizinga imeutikisa mji mkuu wa Somalia-Mogadishu usiku mzima hadi mapema asubuhi ya leo.Raia zaidi wameuwawa na mamia kadhaa, wanakimbiza roho zao wakijaribu kuuhama mji huo.Hili ni wimbi kubwa la kuhama wasomali tangu kupinduliwa kwa dikteta Siad Barre,1991.

„kuna vifo vingi.Nimepakia maiti 2 za jamaa zangu hivi sasa ndani ya motokaa“ alinukuliwa msomali mmoja aliefadhahika kusema.

Mapigano yameripuka tangu jumatano kati ya vikosi vya Somali na Ethiopia dhidi ya waasi wa kiislamu .Watu 131 wanaripotiwa kuuwawa.UM umeripoti kwamba wasomali 321,000 wameihama Somalia tangu Februari,mwaka huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com