1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Daktari wa maradhi ya binaadamu aliyegeuka mwanasiasa

Salim Said Salim3 Novemba 2010

Dk. Ali Mohamed Shein aliibuka na kung'ara katika medani ya kimataifa ya kisiasa miaka tisa iliopita, siku chache baada ya kifo cha ghafla cha aliyekuwa Makamo wa Rais wa Tanzania, Dk. Omar Ali Juma.

https://p.dw.com/p/Pw7X
Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed SheinPicha: DW

Wakati ule jina la Dk. Shein halikuwemo katika orodha ndefu ya watu waliofikiriwa kuchukuwa nafasi ya marehemu Dk. Omar na haikushangaza kusikia watu pale Dk.Shein alipotangazwa kushika wadhifa huo kusikia watu wakiuliza :Ni nani mtu huyu na ametokea wapi?

Kabla ya kunyanyuliwa kushika wadhifa huu wa kuwa msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano , Dk. Shein alikuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jami wa Serikali ya Mapnduzi Zanzibara na ndio kwanza alikuwa anajifunza stadi na mbinu za siasa chafu za uhasama za Visiwani ambazo msomi huwa hajapata nafasi ya kuziona alipokuwa shule.

Huyu ni mtu ambaye huzungumza kwa upole, lakini marafiki zake wa karibu wanasema licha ya huo upole ni mtu asiyependa mzaha hasa kwa masuala ya kazi wanasema ukimya ndio tabia yake. Kwa kawaida Dk. Shein hupenda zaidi kusikiliza watu wanasema nini na sio watu kumsikiliza yeye anasema nini.

Dk. Shein anaonekana kama mtu ambaye si mzungumzaji mwenye mvuto na lugha yenye bashasha na amekuwa akitambulika zaidi kama msomi kuliko mwana siasa na kujipatia sifa ya kupendelea zaidi kukaa pembeni panapokuwepo suitafahamu kuliko kujitumbukiza katikati na kuwa sehemu ya tatizo kwa njia moja au nyengine.

Dk. Shein , sasa akiwa na miaka 62 , ambaye pia anatoka kisiwa cha Pemba, kama watu wote wengine sita waliogombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi huu, ameingia katika medani ya siasa kwa kuombwa na kushajiishwa na sio kwa mapenzi yake mwenyewe. Alipata elimu yake ya msingi na sekondati katika kisiwa cha Unguja na zama zile alitamba sana katika riadha, hasa mbio masafa mafupi.

Ni daktari kitaaluma na analipata shahada ya udaktari (PHD) ya fani kemikia na magonjwa ya binaadamu katika Cho Kikuu cha Newcastle , Uingereza. Alirudi Zanzibar na kufanya kazi kama mkuu wa maabara katika Hospitali ya England.

Alirudi Zanzibar na kufanya kazi kama mkuu wa maabara katika hospitali ya Mnazimoja ambayo ipo masafa mafupi kutoka Ikulu ya Zanzibar. Katika mwaka 1988 alichaguliwa mkuu wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi Zanzibar.

Dk. Shein aliingia katika siasa kwa kuombwa na sio kwa mapenzi yake baada ya baaadhi ya viongozi wa siasa kumtaka aingie kwenye siasa pale upepo wa mageuzi wa kuelekea kwenye mfumo wa vyama vingi vya kisiasa ulipovuma katika visiwa hivi vya karafuu vya Afrika Mashariki katika mwaka1992 wakati wasomi wengi kutoka Pemba wakiwa wameamua kujiunga na chama cha upinzani cha CUF.

Aligombania kiti cha Baraza la Wawakilishi katika jimbo la Mkanyageni alipozaliwa katika uchaguzi wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi katika mwaka 1995, lakini alishindwa na mgombea wa chama cha CUF, kama wenzake wote 20 waliokuwa wagombea wa CCM kule Pemba.

Hata hivyo, alichaguliwa na Rais Salmin Amour Juma ambaye alipta ushindi mwembamba katika uchaguzi wa Rais uliotiliwa mashaka na wachunguzi wa uchaguzi wa ndani nje kama mmoja wa wateuzi wake 10 wa kingia Baraza la Wawakilishi kwa mamlaka aliyopea kikatiba na baadaye kuchaguliwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.

Lakini kwa muda mrefu Dk. Shein alikaa nyuma pale ilipotokea migongano kati ya waliokuwa mahasimu wakuu wa kisiasa, CCM na CUF, ambao kwa miongo miwili uligubika kila kitu katika visiwa hivi ambavyo vilikuwa vikisifika kama vya usalama na shwari.

Dk. Shein ni mtu anayetetea muungano wa serikali mbili na kutaka mafuta yaingizwe katika orodha ya mambo ya Muungano wakati Hamad na chama chake wamesema wanataka Mungano wa serikali ya tatu na mafuta yasiwemo katika orodha ya Muungano na Zanzibar iwe na uhuru wa kuyatumia katika njia inayoona ni kwa maslahi ya watu wake.

Jee ni kwa namna gani DK.Shein na Hamad wataweza kufanya kazi pamoja ni suala linalosubiriwa kwa hamu, lakini dalili zilizoonekana baada ya matokeo ya uchaguzi wa Rais kutolewa na Maalim Seif kumpongeza DK. Shein kwa ushindi na wote kueleza anaweka maslahi ya Zanzibar mbele kunatoa mwanga wa matumaini, lakini wakati ndio utatupa picha halisi. Tusubiri tutaona.

Mwandishi: Salim Said Salim
Mhariri: Oummilkheir Hamidou